×

Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio 9:117 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Taubah ⮕ (9:117) ayat 117 in Swahili

9:117 Surah At-Taubah ayat 117 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 117 - التوبَة - Page - Juz 11

﴿لَّقَد تَّابَ ٱللَّهُ عَلَى ٱلنَّبِيِّ وَٱلۡمُهَٰجِرِينَ وَٱلۡأَنصَارِ ٱلَّذِينَ ٱتَّبَعُوهُ فِي سَاعَةِ ٱلۡعُسۡرَةِ مِنۢ بَعۡدِ مَا كَادَ يَزِيغُ قُلُوبُ فَرِيقٖ مِّنۡهُمۡ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡۚ إِنَّهُۥ بِهِمۡ رَءُوفٞ رَّحِيمٞ ﴾
[التوبَة: 117]

Mwenyezi Mungu amekwisha pokea toba ya Nabii na Wahajiri na Ansari walio mfuata katika saa ya dhiki, pale baada ya kukaribia nyoyo za baadhi yao kugeuka. Basi akapokea toba yao, kwani hakika Yeye kwao wao ni Mpole na ni Mwenye kuwarehemu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: لقد تاب الله على النبي والمهاجرين والأنصار الذين اتبعوه في ساعة العسرة, باللغة السواحيلية

﴿لقد تاب الله على النبي والمهاجرين والأنصار الذين اتبعوه في ساعة العسرة﴾ [التوبَة: 117]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Mwenyezi Mungu Alimuelekeza Nabii Wake Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, kurudi Kwake na kumtii, na Aliwakubalia toba Muhājirūn, waliogura nyumba zao na jamaa zao wakaenda kwenye Nyumba ya Uislamu, na pia Aliwakubalia toba waliomuhami Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, waliotoka pamoja na yeye kupambana na maadui katika vita vya Tabūk katika kipindi cha joto kali na shida ya chakula na vipando. Mwenyezi Mungu Aliwakubalia toba yao baada ya hali kufikia kiwango kwamba nyoyo za baadhi yao zilikaribia kuiyepuka haki na kupendelea ulegevu na utulivu. Lakini Mwenyezi Mungu Aliwathibitisha na Akawapa nguvu na Akawakubalia toba. Hakika Yeye kwao ni Mwingi wa upole ni mwenye huruma. Na miongoni mwa huruma Yake kwao ni kwamba Aliwapa neema ya kutubia, Akaikubali toba yao na Akawathibitisha juu yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek