Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 118 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَعَلَى ٱلثَّلَٰثَةِ ٱلَّذِينَ خُلِّفُواْ حَتَّىٰٓ إِذَا ضَاقَتۡ عَلَيۡهِمُ ٱلۡأَرۡضُ بِمَا رَحُبَتۡ وَضَاقَتۡ عَلَيۡهِمۡ أَنفُسُهُمۡ وَظَنُّوٓاْ أَن لَّا مَلۡجَأَ مِنَ ٱللَّهِ إِلَّآ إِلَيۡهِ ثُمَّ تَابَ عَلَيۡهِمۡ لِيَتُوبُوٓاْۚ إِنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلتَّوَّابُ ٱلرَّحِيمُ ﴾
[التوبَة: 118]
﴿وعلى الثلاثة الذين خلفوا حتى إذا ضاقت عليهم الأرض بما رحبت وضاقت﴾ [التوبَة: 118]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na pia Alikubali toba ya wale watu watatu walioachwa nyuma - nao ni Ka‘b mwana wa Mālik, Hilāl mwana wa Umayyah na Murarah mwana wa a-Rabī'-. Wao walijikalisha nyuma wakaacha kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, wakasikitika masikitiko makubwa. Mpaka ilipofikia hadi ya ardhi kuwa dhiki na wao, pamoja na kuwa ni kunjufu, kwa majonzi na majuto kwa sababu ya kujikalisha nyuma kwao, na nafsi zao zikaingiwa na dhiki kwa hamu iliyowapata na wakahakikisha kwamba hakuna mahali pa kuhamia kumkimbia Mwenyezi Mungu isipokuwa ni Kwake, hapo Mwenyezi Mungu, Aliyetakata na sifa za upungufu na kutukuka, Aliwaafikia kwenye utiifu na kurejea kwenye yale yanayomridhisha Yeye. Hakika Yeye ni Ndiye Mwingi wa kukubali toba za waja Wake, Ndiye Mwenye kuwahurumia |