Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 119 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ ٱتَّقُواْ ٱللَّهَ وَكُونُواْ مَعَ ٱلصَّٰدِقِينَ ﴾
[التوبَة: 119]
﴿ياأيها الذين آمنوا اتقوا الله وكونوا مع الصادقين﴾ [التوبَة: 119]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi ambao mlimuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkaitumia sheria Yake! Fuateni maamrisho ya Mwenyezi Mungu na epukeni makatazo Yake katika kila kitu mnachokitenda na mnachokiacha, na kuweni pamoja na wakweli katika Imani zao na ahadi zao na katika kila jambo miongoni mwa mambo yao |