×

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke 9:120 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Taubah ⮕ (9:120) ayat 120 in Swahili

9:120 Surah At-Taubah ayat 120 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 120 - التوبَة - Page - Juz 11

﴿مَا كَانَ لِأَهۡلِ ٱلۡمَدِينَةِ وَمَنۡ حَوۡلَهُم مِّنَ ٱلۡأَعۡرَابِ أَن يَتَخَلَّفُواْ عَن رَّسُولِ ٱللَّهِ وَلَا يَرۡغَبُواْ بِأَنفُسِهِمۡ عَن نَّفۡسِهِۦۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمۡ لَا يُصِيبُهُمۡ ظَمَأٞ وَلَا نَصَبٞ وَلَا مَخۡمَصَةٞ فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَلَا يَطَـُٔونَ مَوۡطِئٗا يَغِيظُ ٱلۡكُفَّارَ وَلَا يَنَالُونَ مِنۡ عَدُوّٖ نَّيۡلًا إِلَّا كُتِبَ لَهُم بِهِۦ عَمَلٞ صَٰلِحٌۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُضِيعُ أَجۡرَ ٱلۡمُحۡسِنِينَ ﴾
[التوبَة: 120]

Haiwafalii watu wa Madina na Mabedui walio jirani zao kubakia nyuma wasitoke na Mtume, wala kujipendelea nafsi zao kuliko yeye. Hayo ni kwa kuwa hakiwapati kiu, wala machofu, wala njaa, kwa ajili ya Njia ya Mwenyezi Mungu, wala hawendi mahali panapo waghadhibisha makafiri, wala hakiwapati chochote kutokana na maadui, ila huandikiwa kuwa ni kitendo chema. Hakika Mwenyezi Mungu haupotezi ujira wa wanao fanya mema

❮ Previous Next ❯

ترجمة: ما كان لأهل المدينة ومن حولهم من الأعراب أن يتخلفوا عن رسول, باللغة السواحيلية

﴿ما كان لأهل المدينة ومن حولهم من الأعراب أن يتخلفوا عن رسول﴾ [التوبَة: 120]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Haikuwa inafaa kwa watu wa mji wa Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, na walio pambizoni mwao miongoni mwa wanaokaa jangwani, kujikalisha nyuma pamoja na watu wao majumbani mwao na kuacha kumfuata Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Na haikuwa inafaa kwao kuzipendelea nafsi zao mapumziko huku Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, yuko kwenye tabu na usumbufu. Hayo ni kwamba wao hawapatikani na kiu wala usumbufu wala njaa kwenye safari yao na jihadi yao katika njia ya Mwenyezi Mungu, na wala hawakanyagi ardhi yoyote ambayo kuikanyaga kwao inawatia hasira makafiri, na wala hawafaulu kumuua au kumshinda adui wa Mwenyezi Mungu na adui wao isipokuwa wataandikiwa, kwa hayo yote, thawabu ya tendo jema. Hakika Mwenyezi Mungu Hapotezi malipo ya muhsinūn: waliofanya wema kwa kukimbilia kwao kufuata amri ya Mwenyezi Mungu na kusimama kwao imara kutekeleza haki Yake inayowalazimu na haki ya viumbe Vyake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek