Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 122 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿۞ وَمَا كَانَ ٱلۡمُؤۡمِنُونَ لِيَنفِرُواْ كَآفَّةٗۚ فَلَوۡلَا نَفَرَ مِن كُلِّ فِرۡقَةٖ مِّنۡهُمۡ طَآئِفَةٞ لِّيَتَفَقَّهُواْ فِي ٱلدِّينِ وَلِيُنذِرُواْ قَوۡمَهُمۡ إِذَا رَجَعُوٓاْ إِلَيۡهِمۡ لَعَلَّهُمۡ يَحۡذَرُونَ ﴾
[التوبَة: 122]
﴿وما كان المؤمنون لينفروا كافة فلولا نفر من كل فرقة منهم طائفة﴾ [التوبَة: 122]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na haikuwa inafaa kwa Waumini watoke wote kupigana na adui yao, pia hailingani na wao wakae wote. Basi si watoke kupigana jihadi, katika kila kundi, watu ambao itapatikana kwao kutosheleza kufikia malengo. Hivyo ili wapate kujifunza, wale waliokaa wasiende vitani, na kujua hukumu mpya za dini ya Mwenyezi Mungu na zile zilizoteremshiwa Mtume Wake, na wapate kuwaonya jamaa zao kwa yale waliojifunza watakaporejea kwao, huenda wao wakajihadhari na adhabu ya Mwenyezi Mungu, kwa kutekeleza maamrisho Yake na kuepuka makatazo Yake |