Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 126 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿أَوَلَا يَرَوۡنَ أَنَّهُمۡ يُفۡتَنُونَ فِي كُلِّ عَامٖ مَّرَّةً أَوۡ مَرَّتَيۡنِ ثُمَّ لَا يَتُوبُونَ وَلَا هُمۡ يَذَّكَّرُونَ ﴾
[التوبَة: 126]
﴿أو لا يرون أنهم يفتنون في كل عام مرة أو مرتين ثم﴾ [التوبَة: 126]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwani hawaoni wanafiki kwamba Mwenyezi Mungu Anawapa mitihani, kwa kuwaletea ukame na matatizo na kwa kuyatoa nje yale wanayoyaficha ya unafiki, mara moja au mara mbili kila mwaka? Kisha wao, pamoja na hayo, hawatubii kutokana na ukafiri wao na unafiki wao, wala hawazingatii wala hawakumbuki aya za Mwenyezi Mungu wazionazo |