Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 127 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَإِذَا مَآ أُنزِلَتۡ سُورَةٞ نَّظَرَ بَعۡضُهُمۡ إِلَىٰ بَعۡضٍ هَلۡ يَرَىٰكُم مِّنۡ أَحَدٖ ثُمَّ ٱنصَرَفُواْۚ صَرَفَ ٱللَّهُ قُلُوبَهُم بِأَنَّهُمۡ قَوۡمٞ لَّا يَفۡقَهُونَ ﴾
[التوبَة: 127]
﴿وإذا ما أنـزلت سورة نظر بعضهم إلى بعض هل يراكم من أحد﴾ [التوبَة: 127]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na iteremshwapo sura, wanafiki huwa wakishiriana kwa macho, kwa kukataa kuteremka kwake, kucheza shere na kuwa na hasira, kwa yale yaliyoteremka humo ya kutaja aibu zao na matendo yao, kisha wanasema, «Je, kuna yoyote anayewaona mkiondoka kwa Mtume?» Iwapo hakuna yoyote aliyewaona huinuka na kuondoka kwa Mtume, rehema na amani zimshukiye, wakiogopa fedheha. Mwenyezi Mungu Amezipindua nyoyo zao Ameziepusha na Imani kwa sababu wao hawaelewi wala hawazingatii |