Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 22 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿خَٰلِدِينَ فِيهَآ أَبَدًاۚ إِنَّ ٱللَّهَ عِندَهُۥٓ أَجۡرٌ عَظِيمٞ ﴾
[التوبَة: 22]
﴿خالدين فيها أبدا إن الله عنده أجر عظيم﴾ [التوبَة: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hali ya kukaa kwenye mabustani hayo ya Pepo neema hizo kikao kisicho na kikomo. Na hayo ni malipo ya yale waliyoyatanguliza ya utiifu na vitendo vyema katika maisha yao ya ulimwenguni. Hakika Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Ana malipo makubwa kwa aliyeamini na akafanya mema kwa kuzifuata amri Zake na kuyaepuka Makatazo Yake |