Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 35 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿يَوۡمَ يُحۡمَىٰ عَلَيۡهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَتُكۡوَىٰ بِهَا جِبَاهُهُمۡ وَجُنُوبُهُمۡ وَظُهُورُهُمۡۖ هَٰذَا مَا كَنَزۡتُمۡ لِأَنفُسِكُمۡ فَذُوقُواْ مَا كُنتُمۡ تَكۡنِزُونَ ﴾
[التوبَة: 35]
﴿يوم يحمى عليها في نار جهنم فتكوى بها جباههم وجنوبهم وظهورهم هذا﴾ [التوبَة: 35]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Siku ya Kiyama yatawekwa mapande ya dhahabu na fedha kwenye Moto, na yataposhika moto sana, watachomwa nayo, hao wenyewe, nyuso zao, mbavu zao na migongo yao. Na wataambiwa kwa kuwaumbua, «Haya ndiyo mali yenu mliyoyakumbatia na mkazuia, katika mali hayo, haki za Mwenyezi Mungu. Basi onjeni adhabu iumizayo, kwa sababu ya kukusanya kwenu na kuzuia |