×

Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili 9:36 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Taubah ⮕ (9:36) ayat 36 in Swahili

9:36 Surah At-Taubah ayat 36 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 36 - التوبَة - Page - Juz 10

﴿إِنَّ عِدَّةَ ٱلشُّهُورِ عِندَ ٱللَّهِ ٱثۡنَا عَشَرَ شَهۡرٗا فِي كِتَٰبِ ٱللَّهِ يَوۡمَ خَلَقَ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلۡأَرۡضَ مِنۡهَآ أَرۡبَعَةٌ حُرُمٞۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُۚ فَلَا تَظۡلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُمۡۚ وَقَٰتِلُواْ ٱلۡمُشۡرِكِينَ كَآفَّةٗ كَمَا يُقَٰتِلُونَكُمۡ كَآفَّةٗۚ وَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّ ٱللَّهَ مَعَ ٱلۡمُتَّقِينَ ﴾
[التوبَة: 36]

Hakika idadi ya miezi kwa Mwenyezi Mungu ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Mwenyezi Mungu tangu alipo umba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo. Na piganeni na washirikina wote kama wao wnavyo pigana nanyi nyote. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu yu pamoja na wachamngu

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إن عدة الشهور عند الله اثنا عشر شهرا في كتاب الله يوم, باللغة السواحيلية

﴿إن عدة الشهور عند الله اثنا عشر شهرا في كتاب الله يوم﴾ [التوبَة: 36]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Hakika idadi ya miezi, katika hukumu ya Mwenyezi Mungu na kulingana na ilivyoandikwa kwenye al-Lawḥ al-Maḥfūẓ (Ubao Uiohifadhiwa), ni miezi kumi na mbili, tangu siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, kuna minne mitakatifu ambayo Mwenyezi Mungu Ameharamisha ndani yake kupigana. Nayo ni Mfungopili, Mfungotatu, Mfungone na Rajabu. Hiyo ndyo Dini iliyolingana sawa. Basi ndani ya miezi hiyo msizidhulumu nafsi zenu, kwa kuwa uharamu wake umeongezwa. Na kwa kuwa kudhulumu katika miezi hiyo ni kubaya zaidi kuliko katika miezi mingineyo, haina maana kwamba kudhulumu katika miezi mingine kunaruhusiwa. Na wapigeni vita washirikina wote kama wanavyowapiga vita nyote. Na mjue kwamba Mwenyezi Mungu Yuko pamoja na wenye taqwā (uchajimungu) kwa msaada Wake na nusura Yake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek