Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 34 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿۞ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِنَّ كَثِيرٗا مِّنَ ٱلۡأَحۡبَارِ وَٱلرُّهۡبَانِ لَيَأۡكُلُونَ أَمۡوَٰلَ ٱلنَّاسِ بِٱلۡبَٰطِلِ وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ ٱللَّهِۗ وَٱلَّذِينَ يَكۡنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلۡفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرۡهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٖ ﴾
[التوبَة: 34]
﴿ياأيها الذين آمنوا إن كثيرا من الأحبار والرهبان ليأكلون أموال الناس بالباطل﴾ [التوبَة: 34]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Enyi mliomuamini Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na mkazifuata sheria Zake kivitendo, hakika wengi wa wanavyuoni wa watu waliopewa Vitabu na watu wema wao wanakula mali za watu kwa njia isiyokuwa ya haki, kama hongo na vinginevyo, na wanakataza watu wasiingie kwenye Uislamu na wanazuia njia ya Mwenyezi Mungu isifuatwe. Na wale wanaozuia mali wakawa hawatekelezi Zaka zake wala hawatoi katika mali hizo haki za lazima, basi wape bishara ya adhabu iumizayo |