Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 4 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿إِلَّا ٱلَّذِينَ عَٰهَدتُّم مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ ثُمَّ لَمۡ يَنقُصُوكُمۡ شَيۡـٔٗا وَلَمۡ يُظَٰهِرُواْ عَلَيۡكُمۡ أَحَدٗا فَأَتِمُّوٓاْ إِلَيۡهِمۡ عَهۡدَهُمۡ إِلَىٰ مُدَّتِهِمۡۚ إِنَّ ٱللَّهَ يُحِبُّ ٱلۡمُتَّقِينَ ﴾
[التوبَة: 4]
﴿إلا الذين عاهدتم من المشركين ثم لم ينقصوكم شيئا ولم يظاهروا عليكم﴾ [التوبَة: 4]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na wanavuliwa, kwenye hukumu iliyopita, washirikina walioingia pamoja na nyinyi kwenye makubaliano yenye muda ujulikanao, na wakawa hawakufanya hiana kwenye mapatano, wala hawakumsaidia yoyote katika maadui, basi watimizie ahadi yao mpaka mwisho wake uliowekwa Hakika Mwenyezi Mungu Anawapenda wachamungu ambao wanatekeleza waliyoamrishwa. Na ogopeni ushirikina na uhaini na maasia mengineyo |