Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 3 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَأَذَٰنٞ مِّنَ ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦٓ إِلَى ٱلنَّاسِ يَوۡمَ ٱلۡحَجِّ ٱلۡأَكۡبَرِ أَنَّ ٱللَّهَ بَرِيٓءٞ مِّنَ ٱلۡمُشۡرِكِينَ وَرَسُولُهُۥۚ فَإِن تُبۡتُمۡ فَهُوَ خَيۡرٞ لَّكُمۡۖ وَإِن تَوَلَّيۡتُمۡ فَٱعۡلَمُوٓاْ أَنَّكُمۡ غَيۡرُ مُعۡجِزِي ٱللَّهِۗ وَبَشِّرِ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴾
[التوبَة: 3]
﴿وأذان من الله ورسوله إلى الناس يوم الحج الأكبر أن الله بريء﴾ [التوبَة: 3]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na ni ujulisho kutoka kwa Mwenyezi Mungu na ni onyo kwa watu siku ya kuchinja kwamba Mwenyezi Mungu Amejitenga na washirikina; na Mtume Wake pia Amejitenga na wao. Basi ikiwa mtarudi kwenye haki, enyi washirikina, na mkauacha ushirikina wenu, hilo ni bora kwenu. Na mkiipa mgongo haki kwa kutoukubali na mkakataa kuingia kwenye dini ya Mwenyezi Mungu, basi jueni kwamba nyinyi hamtaiponyoka adhabu ya Mwenyezi Mungu. Na waonye, ewe Mtume, hawa wenye kuupa mgongo Uislamu, adhabu ya Mwenyezi Mungu iumizayo |