Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 46 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿۞ وَلَوۡ أَرَادُواْ ٱلۡخُرُوجَ لَأَعَدُّواْ لَهُۥ عُدَّةٗ وَلَٰكِن كَرِهَ ٱللَّهُ ٱنۢبِعَاثَهُمۡ فَثَبَّطَهُمۡ وَقِيلَ ٱقۡعُدُواْ مَعَ ٱلۡقَٰعِدِينَ ﴾
[التوبَة: 46]
﴿ولو أرادوا الخروج لأعدوا له عدة ولكن كره الله انبعاثهم فثبطهم وقيل﴾ [التوبَة: 46]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau wanafiki walitaka kutoka pamoja na wewe, ewe Nabii, kwenye jihadi, basi wangalijiandaa kwa matayarisho ya vyakula na vipando. Lakini Mwenyezi Mungu Amechukia kutoka kwao, ndipo ikawa ni uzito kwao kutoka, kwa mapitisho na Makadirio Yake, ingawa kisheria Amewaamrisha, na wakaambiwa, «Bakieni nyuma pamoja na waliokaa miongoni mwa wagonjwa, madhaifu, wanawake na watoto.» |