×

Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa 9:60 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah At-Taubah ⮕ (9:60) ayat 60 in Swahili

9:60 Surah At-Taubah ayat 60 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 60 - التوبَة - Page - Juz 10

﴿۞ إِنَّمَا ٱلصَّدَقَٰتُ لِلۡفُقَرَآءِ وَٱلۡمَسَٰكِينِ وَٱلۡعَٰمِلِينَ عَلَيۡهَا وَٱلۡمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمۡ وَفِي ٱلرِّقَابِ وَٱلۡغَٰرِمِينَ وَفِي سَبِيلِ ٱللَّهِ وَٱبۡنِ ٱلسَّبِيلِۖ فَرِيضَةٗ مِّنَ ٱللَّهِۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ﴾
[التوبَة: 60]

Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni waajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hikima

❮ Previous Next ❯

ترجمة: إنما الصدقات للفقراء والمساكين والعاملين عليها والمؤلفة قلوبهم وفي الرقاب والغارمين وفي, باللغة السواحيلية

﴿إنما الصدقات للفقراء والمساكين والعاملين عليها والمؤلفة قلوبهم وفي الرقاب والغارمين وفي﴾ [التوبَة: 60]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Zaka za lazima zinapewa wahitaji wasiomiliki kitu, masikini wasiomiliki kiwango kinachowatosha kwa mahitaji yao, wenye kuzishughulikia kwa kuzikusanya,wale ambao mwazizoeza nyoyo zao, miongoni mwa wale mnaotarajia wasilimu au ipate nguvu Imani yao au wawe na manufaa kwa Waislamu au mzuie kwazo madhara ya mtu yoyote yasiwafikie Waislamu. Pia zinatolewa katika kuacha huru watumwa na wale wenye mikataba ya uhuru. Na zinatolewa kupewa wenye kuingia kwenye madeni kwa sababu ya kuleta maelewano baina ya watu na wenye kulemewa na madeni waliyokopa kwa lengo lisiliokuwa la uharibifu au utumiaji wa kupita kiasi kisha wakashindwa kulipa. Na zinapewa wapiganaji katika njia ya Mwenyezi Mungu. Na zinapewa msafiri aliyeishiwa na matumizi. Ugawaji huu ni lazima Aliyoifaradhia Mwenyezi Mungu na Akaikadiria. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi mno wa mambo yanayowafaa waja Wake, ni Mwingi wa hekima katika uendeshaji mambo Wake na sheria Zake
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek