Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 61 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿وَمِنۡهُمُ ٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ ٱلنَّبِيَّ وَيَقُولُونَ هُوَ أُذُنٞۚ قُلۡ أُذُنُ خَيۡرٖ لَّكُمۡ يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَيُؤۡمِنُ لِلۡمُؤۡمِنِينَ وَرَحۡمَةٞ لِّلَّذِينَ ءَامَنُواْ مِنكُمۡۚ وَٱلَّذِينَ يُؤۡذُونَ رَسُولَ ٱللَّهِ لَهُمۡ عَذَابٌ أَلِيمٞ ﴾
[التوبَة: 61]
﴿ومنهم الذين يؤذون النبي ويقولون هو أذن قل أذن خير لكم يؤمن﴾ [التوبَة: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Miongoni mwa wanafiki kuna watu wanaomkera Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa maneno na wanasema, «Yeye anasikiliza kila aambiwalo na analiamini.» Waambie, «Muhammad ni sikio linalosikiliza kila jema. Anamuamini Mwenyezi Mungu na anawasadiki Waumini kwa yale wanayomwambia. Na yeye ni rehema kwa aliyemfuata na akaongoka kwa uongofu Wake. Na wenye kumkera Mtume wa Mwenyezi Mungu, Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, kwa namna yoyote ya kumkera, watakuwa na adhabu yenye kuumiza |