Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 87 - التوبَة - Page - Juz 10
﴿رَضُواْ بِأَن يَكُونُواْ مَعَ ٱلۡخَوَالِفِ وَطُبِعَ عَلَىٰ قُلُوبِهِمۡ فَهُمۡ لَا يَفۡقَهُونَ ﴾
[التوبَة: 87]
﴿رضوا بأن يكونوا مع الخوالف وطبع على قلوبهم فهم لا يفقهون﴾ [التوبَة: 87]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wanafiki hawa wameridhika na aibu, nayo ni kukaa majumbani pamoja na wanawake na watoto na wenye nyudhuru. Na Mwenyezi Mungu Amezipiga muhuri nyoyo zao kwa sababu ya unafiki wao na kujiweka kwao nyuma kuacha jihadi na kutoka pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, katika njia ya Mwenyezi Mungu. Wao hawayaelewi yale ambayo yana maslahi yao na uongofu wao |