Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 97 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿ٱلۡأَعۡرَابُ أَشَدُّ كُفۡرٗا وَنِفَاقٗا وَأَجۡدَرُ أَلَّا يَعۡلَمُواْ حُدُودَ مَآ أَنزَلَ ٱللَّهُ عَلَىٰ رَسُولِهِۦۗ وَٱللَّهُ عَلِيمٌ حَكِيمٞ ﴾
[التوبَة: 97]
﴿الأعراب أشد كفرا ونفاقا وأجدر ألا يعلموا حدود ما أنـزل الله على﴾ [التوبَة: 97]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mabedui, wakazi wa jangwani, ni washupavu zaidi wa ukafiri na unafiki kuliko wakazi wa mjini. Hivyo ni kwa sababu ya ugumu wa tabia za, ususuavu wa nyoyo zao na kuwa mbali kwao na elimu, wanavyuoni, vikao vya mawaidha na dhikr (kumtaja Mwenyezi Mungu). Kwa hivyo wao wanastahilii zaidi wasijue mipaka ya Dini na zile sheria na hukumu ambazo Mwenyezi Mungu Ameziteremsha. Na Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa hali za hawa wote, ni Mwenye hekima Katika uendeshaji Wake mambo ya waja Wake |