Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 98 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ مَغۡرَمٗا وَيَتَرَبَّصُ بِكُمُ ٱلدَّوَآئِرَۚ عَلَيۡهِمۡ دَآئِرَةُ ٱلسَّوۡءِۗ وَٱللَّهُ سَمِيعٌ عَلِيمٞ ﴾
[التوبَة: 98]
﴿ومن الأعراب من يتخذ ما ينفق مغرما ويتربص بكم الدوائر عليهم دائرة﴾ [التوبَة: 98]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miogoni mwa Mabedui kuna wanaohesabu wanachokitoa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni kodi na ni hasara, hawatazamii, kwa kile wakitoacho, thawabu wala kujikinga na adhabu, na wana hamu mupatwe na misiba na maafa. Lakini mabaya yatawazunguka wao, sio Waislamu. Na Mwenyezi Mungu ni Msikizi wa wanayoyasema, ni Mjuzi wa nia zao mbaya |