Quran with Swahili translation - Surah At-Taubah ayat 99 - التوبَة - Page - Juz 11
﴿وَمِنَ ٱلۡأَعۡرَابِ مَن يُؤۡمِنُ بِٱللَّهِ وَٱلۡيَوۡمِ ٱلۡأٓخِرِ وَيَتَّخِذُ مَا يُنفِقُ قُرُبَٰتٍ عِندَ ٱللَّهِ وَصَلَوَٰتِ ٱلرَّسُولِۚ أَلَآ إِنَّهَا قُرۡبَةٞ لَّهُمۡۚ سَيُدۡخِلُهُمُ ٱللَّهُ فِي رَحۡمَتِهِۦٓۚ إِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٞ رَّحِيمٞ ﴾
[التوبَة: 99]
﴿ومن الأعراب من يؤمن بالله واليوم الآخر ويتخذ ما ينفق قربات عند﴾ [التوبَة: 99]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na miongoni mwa Mabedui kuna wanaomuamini Mwenyezi Mungu na kukubali upweke Wake, kufufuliwa baada ya kufa na kuwa kuna thawabu na adhabu, na wanatarajia malipo mema kwa kile chochote wanachokitoa cha matumizi katika kupigana jihadi na washirikina, kwa kusudia radhi za Mwenyezi Mungu na mapenzi Yake, na kukifanya ni njia ya kumfanya apate maombi ya Mtume, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye. Jua utanabahi kwamba matendo haya yatawaweka wao karibu na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka. Mwenyezi Mungu Atawatia kwenye Pepo Yake. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa msamaha wa maovu waliyoyafanya, ni Mwenye kuwarehemu |