The Quran in Swahili - Surah Inshiqaq translated into Swahili, Surah Al-Inshiqaq in Swahili. We provide accurate translation of Surah Inshiqaq in Swahili - السواحيلية, Verses 25 - Surah Number 84 - Page 589.
إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ (1) Itapo chanika mbingu |
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (2) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza |
وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ (3) Na ardhi itakapo tanuliwa |
وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ (4) Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu |
وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (5) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza |
يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ (6) Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta |
فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ (7) Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia |
فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا (8) Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi |
وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا (9) Na arudi kwa ahali zake na furaha |
وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ (10) Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake |
فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا (11) Basi huyo ataomba kuteketea |
وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا (12) Na ataingia Motoni |
إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا (13) Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake |
إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ (14) Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena |
بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا (15) Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona |
فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ (16) Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa |
وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ (17) Na kwa usiku na unavyo vikusanya |
وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ (18) Na kwa mwezi unapo pevuka |
لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ (19) Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka |
فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (20) Basi wana nini hawaamini |
وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩ (21) Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu |
بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ (22) Bali walio kufuru wanakanusha tu |
وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ (23) Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria |
فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (24) Basi wabashirie adhabu chungu |
إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ (25) Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika |