The Quran in Swahili - Surah Mutaffifin translated into Swahili, Surah Al-Mutaffifin in Swahili. We provide accurate translation of Surah Mutaffifin in Swahili - السواحيلية, Verses 36 - Surah Number 83 - Page 587.

| وَيْلٌ لِّلْمُطَفِّفِينَ (1) Ole wao hao wapunjao |
| الَّذِينَ إِذَا اكْتَالُوا عَلَى النَّاسِ يَسْتَوْفُونَ (2) Ambao wanapo jipimia kwa watu hudai watimiziwe |
| وَإِذَا كَالُوهُمْ أَو وَّزَنُوهُمْ يُخْسِرُونَ (3) Na wao wanapo wapimia watu kwa kipimo au mizani hupunguza |
| أَلَا يَظُنُّ أُولَٰئِكَ أَنَّهُم مَّبْعُوثُونَ (4) Kwani hawadhani hao kwamba watafufuliwa |
| لِيَوْمٍ عَظِيمٍ (5) Katika Siku iliyo kuu |
| يَوْمَ يَقُومُ النَّاسُ لِرَبِّ الْعَالَمِينَ (6) Siku watapo msimamia watu Mola Mlezi wa walimwengu wote |
| كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْفُجَّارِ لَفِي سِجِّينٍ (7) Hasha! Hakika maandiko ya wakosefu bila ya shaka yamo katika Sijjin |
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا سِجِّينٌ (8) Unajua nini Sijjin |
| كِتَابٌ مَّرْقُومٌ (9) Kitabu kilicho andikwa |
| وَيْلٌ يَوْمَئِذٍ لِّلْمُكَذِّبِينَ (10) Ole wao siku hiyo kwa wanao kadhibisha |
| الَّذِينَ يُكَذِّبُونَ بِيَوْمِ الدِّينِ (11) Ambao wanaikadhibisha Siku ya Malipo |
| وَمَا يُكَذِّبُ بِهِ إِلَّا كُلُّ مُعْتَدٍ أَثِيمٍ (12) Wala haikadhibishi ila kila mwenye kuruka mipaka, mwenye dhambi |
| إِذَا تُتْلَىٰ عَلَيْهِ آيَاتُنَا قَالَ أَسَاطِيرُ الْأَوَّلِينَ (13) Anapo somewa Aya zetu husema: Ni visa vya watu wa kale |
| كَلَّا ۖ بَلْ ۜ رَانَ عَلَىٰ قُلُوبِهِم مَّا كَانُوا يَكْسِبُونَ (14) Hasha! Bali yametia kutu juu ya nyoyo zao hao walio kuwa wakiyachuma |
| كَلَّا إِنَّهُمْ عَن رَّبِّهِمْ يَوْمَئِذٍ لَّمَحْجُوبُونَ (15) Hasha! Hakika hao siku hiyo bila ya shaka watazuiliwa na neema za Mola wao Mlezi |
| ثُمَّ إِنَّهُمْ لَصَالُو الْجَحِيمِ (16) Kisha wataingia Motoni |
| ثُمَّ يُقَالُ هَٰذَا الَّذِي كُنتُم بِهِ تُكَذِّبُونَ (17) Kisha waambiwe: Haya ndiyo mliyo kuwa mkiyakadhabisha |
| كَلَّا إِنَّ كِتَابَ الْأَبْرَارِ لَفِي عِلِّيِّينَ (18) Hasha! Hakika maandiko ya watu wema bila ya shaka yamo katika I'liyyin |
| وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ (19) Na nini kitakacho kujuvya nini I'liyyin |
| كِتَابٌ مَّرْقُومٌ (20) Kitabu kilicho andikwa |
| يَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ (21) Wanakishuhudia walio karibishwa |
| إِنَّ الْأَبْرَارَ لَفِي نَعِيمٍ (22) Hakika watu wema bila ya shaka watakuwa katika neema |
| عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ (23) Wakae juu ya viti vya enzi wakiangalia |
| تَعْرِفُ فِي وُجُوهِهِمْ نَضْرَةَ النَّعِيمِ (24) Utatambua katika nyuso zao mng'aro wa neema |
| يُسْقَوْنَ مِن رَّحِيقٍ مَّخْتُومٍ (25) Watanyweshwa kinywaji safi kiliyo tiwa muhuri |
| خِتَامُهُ مِسْكٌ ۚ وَفِي ذَٰلِكَ فَلْيَتَنَافَسِ الْمُتَنَافِسُونَ (26) Muhuri wake ni miski. Na katika hayo washindanie wenye kushindana |
| وَمِزَاجُهُ مِن تَسْنِيمٍ (27) Na mchanganyiko wake ni Tasniim |
| عَيْنًا يَشْرَبُ بِهَا الْمُقَرَّبُونَ (28) Chemchem watakayo inywa walio kurubishwa |
| إِنَّ الَّذِينَ أَجْرَمُوا كَانُوا مِنَ الَّذِينَ آمَنُوا يَضْحَكُونَ (29) Kwa hakika wale walio kuwa wakosefu walikuwa wakiwacheka walio amini |
| وَإِذَا مَرُّوا بِهِمْ يَتَغَامَزُونَ (30) Na wanapo pita karibu yao wakikonyezana |
| وَإِذَا انقَلَبُوا إِلَىٰ أَهْلِهِمُ انقَلَبُوا فَكِهِينَ (31) Na wanapo rudi kwa watu wao hurudi nao wamefurahi |
| وَإِذَا رَأَوْهُمْ قَالُوا إِنَّ هَٰؤُلَاءِ لَضَالُّونَ (32) Na wanapo waona husema: Hakika hawa ndio khasa walio potea |
| وَمَا أُرْسِلُوا عَلَيْهِمْ حَافِظِينَ (33) Na wao hawakutumwa wawe walinzi juu yao |
| فَالْيَوْمَ الَّذِينَ آمَنُوا مِنَ الْكُفَّارِ يَضْحَكُونَ (34) Basi leo walio amini ndio watawacheka makafiri |
| عَلَى الْأَرَائِكِ يَنظُرُونَ (35) Nao wako juu ya viti vya enzi wakiangalia |
| هَلْ ثُوِّبَ الْكُفَّارُ مَا كَانُوا يَفْعَلُونَ (36) Je! makafiri wamelipwa malipo ya yale waliyo kuwa wakiyatenda |