القرآن باللغة السواحيلية - سورة الانشقاق مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Inshiqaq in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة الانشقاق باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 25 - رقم السورة 84 - الصفحة 589.

| إِذَا السَّمَاءُ انشَقَّتْ (1) Itapo chanika mbingu |
| وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (2) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza |
| وَإِذَا الْأَرْضُ مُدَّتْ (3) Na ardhi itakapo tanuliwa |
| وَأَلْقَتْ مَا فِيهَا وَتَخَلَّتْ (4) Na kuvitoa vilivyo kuwa ndani yake, ikawa tupu |
| وَأَذِنَتْ لِرَبِّهَا وَحُقَّتْ (5) Na ikamsikiliza Mola wake Mlezi, na ikapasiwa kumsikiliza |
| يَا أَيُّهَا الْإِنسَانُ إِنَّكَ كَادِحٌ إِلَىٰ رَبِّكَ كَدْحًا فَمُلَاقِيهِ (6) Ewe mtu! Hakika wewe unajikusuru kwa juhudi kumwendea Mola wako Mlezi, basi utamkuta |
| فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ (7) Ama atakaye pewa daftari lake kwa mkono wa kulia |
| فَسَوْفَ يُحَاسَبُ حِسَابًا يَسِيرًا (8) Basi huyo atahisabiwa hisabu nyepesi |
| وَيَنقَلِبُ إِلَىٰ أَهْلِهِ مَسْرُورًا (9) Na arudi kwa ahali zake na furaha |
| وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ وَرَاءَ ظَهْرِهِ (10) Na ama atakaye pewa daftari lake kwa nyuma ya mgongo wake |
| فَسَوْفَ يَدْعُو ثُبُورًا (11) Basi huyo ataomba kuteketea |
| وَيَصْلَىٰ سَعِيرًا (12) Na ataingia Motoni |
| إِنَّهُ كَانَ فِي أَهْلِهِ مَسْرُورًا (13) Hakika alikuwa furahani kati ya jamaa zake |
| إِنَّهُ ظَنَّ أَن لَّن يَحُورَ (14) Huyo hakika alidhani kuwa hatarejea tena |
| بَلَىٰ إِنَّ رَبَّهُ كَانَ بِهِ بَصِيرًا (15) Kwani? Hakika Mola wake Mlezi alikuwa akimwona |
| فَلَا أُقْسِمُ بِالشَّفَقِ (16) Basi ninaapa kwa wekundu wa jua linapo kuchwa |
| وَاللَّيْلِ وَمَا وَسَقَ (17) Na kwa usiku na unavyo vikusanya |
| وَالْقَمَرِ إِذَا اتَّسَقَ (18) Na kwa mwezi unapo pevuka |
| لَتَرْكَبُنَّ طَبَقًا عَن طَبَقٍ (19) Lazima mtapanda t'abaka kwa t'abaka |
| فَمَا لَهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ (20) Basi wana nini hawaamini |
| وَإِذَا قُرِئَ عَلَيْهِمُ الْقُرْآنُ لَا يَسْجُدُونَ ۩ (21) Na wanapo somewa Qur'ani hawasujudu |
| بَلِ الَّذِينَ كَفَرُوا يُكَذِّبُونَ (22) Bali walio kufuru wanakanusha tu |
| وَاللَّهُ أَعْلَمُ بِمَا يُوعُونَ (23) Na Mwenyezi Mungu anajua wanayo yadhamiria |
| فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ (24) Basi wabashirie adhabu chungu |
| إِلَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ أَجْرٌ غَيْرُ مَمْنُونٍ (25) Isipo kuwa wale walio amini na wakatenda mema; hao watakuwa na ujira usio malizika |