القرآن باللغة السواحيلية - سورة الفجر مترجمة إلى اللغة السواحيلية، Surah Fajr in Swahili. نوفر ترجمة دقيقة سورة الفجر باللغة السواحيلية - Swahili, الآيات 30 - رقم السورة 89 - الصفحة 593.

| وَالْفَجْرِ (1) Naapa kwa alfajiri |
| وَلَيَالٍ عَشْرٍ (2) Na kwa masiku kumi |
| وَالشَّفْعِ وَالْوَتْرِ (3) Na kwa viwili viwili na kimoja kimoja |
| وَاللَّيْلِ إِذَا يَسْرِ (4) Na kwa usiku unapo pita |
| هَلْ فِي ذَٰلِكَ قَسَمٌ لِّذِي حِجْرٍ (5) Je! Hapana katika haya kiapo kwa mwenye akili |
| أَلَمْ تَرَ كَيْفَ فَعَلَ رَبُّكَ بِعَادٍ (6) Kwani hukuona jinsi Mola wako Mlezi alivyo wafanya kina A'di |
| إِرَمَ ذَاتِ الْعِمَادِ (7) Wa Iram, wenye majumba marefu |
| الَّتِي لَمْ يُخْلَقْ مِثْلُهَا فِي الْبِلَادِ (8) Ambao haukuumbwa mfano wake katika nchi |
| وَثَمُودَ الَّذِينَ جَابُوا الصَّخْرَ بِالْوَادِ (9) Na Thamudi walio chonga majabali huko bondeni |
| وَفِرْعَوْنَ ذِي الْأَوْتَادِ (10) Na Firauni mwenye vigingi |
| الَّذِينَ طَغَوْا فِي الْبِلَادِ (11) Ambao walifanya jeuri katika nchi |
| فَأَكْثَرُوا فِيهَا الْفَسَادَ (12) Wakakithirisha humo ufisadi |
| فَصَبَّ عَلَيْهِمْ رَبُّكَ سَوْطَ عَذَابٍ (13) Basi Mola wako Mlezi aliwapiga mjeledi wa adhabu |
| إِنَّ رَبَّكَ لَبِالْمِرْصَادِ (14) Hakika Mola wako Mlezi yupo kwenye mavizio anawavizia |
| فَأَمَّا الْإِنسَانُ إِذَا مَا ابْتَلَاهُ رَبُّهُ فَأَكْرَمَهُ وَنَعَّمَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَكْرَمَنِ (15) Ama mtu anapo jaribiwa na Mola wake Mlezi, akamkirimu na akamneemesha, husema: Mola wangu Mlezi amenikirimu |
| وَأَمَّا إِذَا مَا ابْتَلَاهُ فَقَدَرَ عَلَيْهِ رِزْقَهُ فَيَقُولُ رَبِّي أَهَانَنِ (16) Na ama anapo mjaribu akampunguzia riziki yake, husema: Mola wangu Mlezi amenitia unyonge |
| كَلَّا ۖ بَل لَّا تُكْرِمُونَ الْيَتِيمَ (17) Sivyo hivyo! Bali nyinyi hamuwakirimu mayatima |
| وَلَا تَحَاضُّونَ عَلَىٰ طَعَامِ الْمِسْكِينِ (18) Wala hamhimizani kulisha masikini |
| وَتَأْكُلُونَ التُّرَاثَ أَكْلًا لَّمًّا (19) Na mnakula urithi kwa ulaji wa pupa |
| وَتُحِبُّونَ الْمَالَ حُبًّا جَمًّا (20) Na mnapenda mali pendo la kupita kiasi |
| كَلَّا إِذَا دُكَّتِ الْأَرْضُ دَكًّا دَكًّا (21) Sivyo hivyo! Itakapo vunjwa ardhi vipande vipande |
| وَجَاءَ رَبُّكَ وَالْمَلَكُ صَفًّا صَفًّا (22) Na akaja Mola wako Mlezi na Malaika safu safu |
| وَجِيءَ يَوْمَئِذٍ بِجَهَنَّمَ ۚ يَوْمَئِذٍ يَتَذَكَّرُ الْإِنسَانُ وَأَنَّىٰ لَهُ الذِّكْرَىٰ (23) Na ikaletwa Jahannamu siku hiyo, siku hiyo mtu atakumbuka! Lakini kukumbuka huko kutamfaa nini |
| يَقُولُ يَا لَيْتَنِي قَدَّمْتُ لِحَيَاتِي (24) Atasema: Laiti ningeli jitangulizia kwa uhai wangu |
| فَيَوْمَئِذٍ لَّا يُعَذِّبُ عَذَابَهُ أَحَدٌ (25) Basi siku hiyo hataadhibu yeyote namna ya kuadhibu kwake |
| وَلَا يُوثِقُ وَثَاقَهُ أَحَدٌ (26) Wala hatafunga yeyote kama kufunga kwake |
| يَا أَيَّتُهَا النَّفْسُ الْمُطْمَئِنَّةُ (27) Ewe nafsi iliyo tua |
| ارْجِعِي إِلَىٰ رَبِّكِ رَاضِيَةً مَّرْضِيَّةً (28) Rejea kwa Mola wako Mlezi umeridhika, na umemridhisha |
| فَادْخُلِي فِي عِبَادِي (29) Basi ingia miongoni mwa waja wangu |
| وَادْخُلِي جَنَّتِي (30) Na ingia katika Pepo yangu |