Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 109 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَٱتَّبِعۡ مَا يُوحَىٰٓ إِلَيۡكَ وَٱصۡبِرۡ حَتَّىٰ يَحۡكُمَ ٱللَّهُۚ وَهُوَ خَيۡرُ ٱلۡحَٰكِمِينَ ﴾
[يُونس: 109]
﴿واتبع ما يوحى إليك واصبر حتى يحكم الله وهو خير الحاكمين﴾ [يُونس: 109]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na uufuate, ewe Mtume, wahyi wa Mwenyezi Mungu Aliokutumia wewe na uutumie kivitendo. Na uwe na subira katika kumtii Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na katika kujiepusha na mambo ya kumuasi na kwa kuvumilia makero ya wenye kukukera katika kuufikisha ujumbe Wake, mpaka Mwenyezi Mungu Atoe uamuzi Wake kwao na kwako. Na Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu, Ndiye mbora wa kutoa uamuzi, kwa kuwa uamuzi Wake unakusanya uadilifu uliokamilika |