Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 108 - يُونس - Page - Juz 11
﴿قُلۡ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ قَدۡ جَآءَكُمُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكُمۡۖ فَمَنِ ٱهۡتَدَىٰ فَإِنَّمَا يَهۡتَدِي لِنَفۡسِهِۦۖ وَمَن ضَلَّ فَإِنَّمَا يَضِلُّ عَلَيۡهَاۖ وَمَآ أَنَا۠ عَلَيۡكُم بِوَكِيلٖ ﴾
[يُونس: 108]
﴿قل ياأيها الناس قد جاءكم الحق من ربكم فمن اهتدى فإنما يهتدي﴾ [يُونس: 108]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Sema, ewe Mtume, kuwaambia hawa watu, «Amewajia nyinyi Mtume wa Mwenyezi Mungu na Qur’ani ambayo ndani yake muna maelezo ya kuwaongoa nyinyi. Basi mwenye kuongoka kwa uongofu wa Mwenyezi Mungu, hakika matunda ya kitendo chake yatamrudia yeye mwenyewe. Na mwenye kupotoka akawa kando na haki na akaendelea kwenye upotevu, hakika upotevu wake na madhara yake yatamshukia yeye mwenyewe. Na mimi si kuwakilishwa kwenu mpaka muwe Waumini. Mimi ni mjumbe mwenye kufikisha , nawafikishia yale niliyotumwa kwayo |