Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 11 - يُونس - Page - Juz 11
﴿۞ وَلَوۡ يُعَجِّلُ ٱللَّهُ لِلنَّاسِ ٱلشَّرَّ ٱسۡتِعۡجَالَهُم بِٱلۡخَيۡرِ لَقُضِيَ إِلَيۡهِمۡ أَجَلُهُمۡۖ فَنَذَرُ ٱلَّذِينَ لَا يَرۡجُونَ لِقَآءَنَا فِي طُغۡيَٰنِهِمۡ يَعۡمَهُونَ ﴾
[يُونس: 11]
﴿ولو يعجل الله للناس الشر استعجالهم بالخير لقضي إليهم أجلهم فنذر الذين﴾ [يُونس: 11]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na lau Mwenyezi Mungu Awaharakishia watu kuyakubali maombi yao ya kujitakia mabaya kama Anavyowaharakishia katika kuwakubalia maombi yao ya kujitakia mazuri wangaliangamia. Hivyo basi tunawaacha, wale ambao hawaogopi mateso yetu wala hawaamini kidhati kufufuliwa na kuhuishwa, ndani ya uasi wao na ujeuri wao hali ya kuwa wanashangaa na kuduwaa |