Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 12 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَإِذَا مَسَّ ٱلۡإِنسَٰنَ ٱلضُّرُّ دَعَانَا لِجَنۢبِهِۦٓ أَوۡ قَاعِدًا أَوۡ قَآئِمٗا فَلَمَّا كَشَفۡنَا عَنۡهُ ضُرَّهُۥ مَرَّ كَأَن لَّمۡ يَدۡعُنَآ إِلَىٰ ضُرّٖ مَّسَّهُۥۚ كَذَٰلِكَ زُيِّنَ لِلۡمُسۡرِفِينَ مَا كَانُواْ يَعۡمَلُونَ ﴾
[يُونس: 12]
﴿وإذا مس الإنسان الضر دعانا لجنبه أو قاعدا أو قائما فلما كشفنا﴾ [يُونس: 12]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na impatapo binadamu shida, anatuomba tumsaidiye katika kumuondolea hiyo akiwa katika hali ya kuwa amelala kwa ubavu wake au ameketi au amesimama, kulingana na hali ile alivyo wakati mashaka yalipomshukia. Na tunapomuondolea ile shida iliyompata, huendelea kuifuata ile njia yake ya mwanzo kabla hajapatwa na mashaka na huyasahau yale aliokuwa nayo ya shida na matatizo na huacha kumshukuru Mola Wake aliyemuondolea yale aliyokuwa nayo ya matatizo. Na kama alivyopambiwa binadamu huyu kuendelea katika kukanusha kwake na kuwa na ujeuri baada ya Mwenyezi Mungu kukuondolea mashaka aliyokuwa nayo , vilevile walipambiwa wale waliopita kiasi katika kumzulia Mwenyezi Mungu urongo na Manabii Wake yale ambayo walikuwa wakiyafanya ya kumuasi Mwenyezi Mungu na kumshirikisha |