Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 13 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَلَقَدۡ أَهۡلَكۡنَا ٱلۡقُرُونَ مِن قَبۡلِكُمۡ لَمَّا ظَلَمُواْ وَجَآءَتۡهُمۡ رُسُلُهُم بِٱلۡبَيِّنَٰتِ وَمَا كَانُواْ لِيُؤۡمِنُواْۚ كَذَٰلِكَ نَجۡزِي ٱلۡقَوۡمَ ٱلۡمُجۡرِمِينَ ﴾
[يُونس: 13]
﴿ولقد أهلكنا القرون من قبلكم لما ظلموا وجاءتهم رسلهم بالبينات وما كانوا﴾ [يُونس: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Hakika tuliwaangamiza watu waliowakanusha Mitume wa Mwenyezi Mungu kabla yenu, enyi mliomshirikisha Mola wenu, waliposhirikisha na wakawajia Mitume wao kutoka kwa Mwenyezi Mungu wakiwa na miujiza iliyo wazi na hoja zenye kubainisha ukweli wa yale aliyekuja nayo. Basi watu hawa hawakuwa ni wenye kuwaamini Mitume wao na kuwafuata, kwa hivyo walistahili maangamivu. Na mfano wa maangamivu hayo ndivyo atakavyolipwa kila mhalifu mwenyekukiuka mipaka ya Mwenyezi Mungu |