Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 20 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَيَقُولُونَ لَوۡلَآ أُنزِلَ عَلَيۡهِ ءَايَةٞ مِّن رَّبِّهِۦۖ فَقُلۡ إِنَّمَا ٱلۡغَيۡبُ لِلَّهِ فَٱنتَظِرُوٓاْ إِنِّي مَعَكُم مِّنَ ٱلۡمُنتَظِرِينَ ﴾
[يُونس: 20]
﴿ويقولون لولا أنـزل عليه آية من ربه فقل إنما الغيب لله فانتظروا﴾ [يُونس: 20]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na makafiri hawa wakaidi wanasema «Basi si ateremshiwe Muhammad ujuzi, dalili na miujiza inayoonekana, kutoka kwa Mola wake, ambayo kwayo tutajua kuwa yeye yuko juu ya haki katika yale anayoyasema.» Waambie, ewe Mtume, «Hakuna ajuwaye ghayb (yasioonekena) isipokuwa ni Mwenyezi Mungu. Akitaka (kufanya wanayoyataka) Atafanya na akitaka (kutofanya) hatafanya. Basi ngojeni, enyi watu, uamuzi wa Mwenyezi Mungu baina yetu na nyinyi wa kuyaharakisha mateso Yake kwa wakosa kati yetu na kumnusuru mwenye haki; mimi nalingojea hilo |