Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 21 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَإِذَآ أَذَقۡنَا ٱلنَّاسَ رَحۡمَةٗ مِّنۢ بَعۡدِ ضَرَّآءَ مَسَّتۡهُمۡ إِذَا لَهُم مَّكۡرٞ فِيٓ ءَايَاتِنَاۚ قُلِ ٱللَّهُ أَسۡرَعُ مَكۡرًاۚ إِنَّ رُسُلَنَا يَكۡتُبُونَ مَا تَمۡكُرُونَ ﴾
[يُونس: 21]
﴿وإذا أذقنا الناس رحمة من بعد ضراء مستهم إذا لهم مكر في﴾ [يُونس: 21]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tunapowaonjesha washirikina usahali, faraja na neema baada ya uzito, shida na dhiki zilizowapata, punde si punde wanakanusha na kuzifanyia shere aya za Mwenyezi Mungu. Sema uwaambie, ewe Mtume, washirikina hawa wanaofanya shere, «Mwenyezi Mungu ni ni mpesi wa vitimbi, kuwavuta nyinyi kidogokidogo na kuwatesa.» Hakika watunzi wetu tunaowatuma kwenu, wanayasajili kwenu yale mnayoyafanyia vitimbi kuhusu aya zetu kisha tutawahesabu kwa hayo |