Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 22 - يُونس - Page - Juz 11
﴿هُوَ ٱلَّذِي يُسَيِّرُكُمۡ فِي ٱلۡبَرِّ وَٱلۡبَحۡرِۖ حَتَّىٰٓ إِذَا كُنتُمۡ فِي ٱلۡفُلۡكِ وَجَرَيۡنَ بِهِم بِرِيحٖ طَيِّبَةٖ وَفَرِحُواْ بِهَا جَآءَتۡهَا رِيحٌ عَاصِفٞ وَجَآءَهُمُ ٱلۡمَوۡجُ مِن كُلِّ مَكَانٖ وَظَنُّوٓاْ أَنَّهُمۡ أُحِيطَ بِهِمۡ دَعَوُاْ ٱللَّهَ مُخۡلِصِينَ لَهُ ٱلدِّينَ لَئِنۡ أَنجَيۡتَنَا مِنۡ هَٰذِهِۦ لَنَكُونَنَّ مِنَ ٱلشَّٰكِرِينَ ﴾
[يُونس: 22]
﴿هو الذي يسيركم في البر والبحر حتى إذا كنتم في الفلك وجرين﴾ [يُونس: 22]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Anayewaendesha nyinyi, enyi watu, juu ya wanyama na vinginevyo barani, na ndani ya majahazi baharini, hata mnapokuwa humo na yakatembea kwa upepo mzuri na abiria wa hayo majahazi wakafurahi kwa huo upepo mzuri, ghafla majahazi hayo yanajiwa na upepo mkali, na mawimbi yakawajia abiria kutoka kila mahali, na wakawa na hakika kuwa maangamivu yamewazunguka, hapo wanamtakasia dua Mwenyezi Mungu Peke Yake, na wakaviacha vile ambavyo walikuwa wakiviabudu na wanasema, «Ukituokoa kutoka kwenye shida hii ambayo tuko nayo, kwa kweli tutakuwa ni miongoni mwa wale wenye kukushukuru kwa neema yako.» |