Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 23 - يُونس - Page - Juz 11
﴿فَلَمَّآ أَنجَىٰهُمۡ إِذَا هُمۡ يَبۡغُونَ فِي ٱلۡأَرۡضِ بِغَيۡرِ ٱلۡحَقِّۗ يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّمَا بَغۡيُكُمۡ عَلَىٰٓ أَنفُسِكُمۖ مَّتَٰعَ ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَاۖ ثُمَّ إِلَيۡنَا مَرۡجِعُكُمۡ فَنُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمۡ تَعۡمَلُونَ ﴾
[يُونس: 23]
﴿فلما أنجاهم إذا هم يبغون في الأرض بغير الحق ياأيها الناس إنما﴾ [يُونس: 23]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mwenyezi Mungu Alipowaondolea shida na mikasa, punde si punde wakawa wanafanya uharibifu na maasia katika ardhi. Enyi watu, hakika ukorofi wa udhalimu wenu unawarudia nyinyi wenyewe. Chukueni starehe katika uhai wa kilimwengu wenye kuondoka, kisha kwetu ndio mwisho wenu na marejeo yenu, hapo tutawapa habari ya matendo yenu yote na tutawahesabu juu ya hayo |