Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 26 - يُونس - Page - Juz 11
﴿۞ لِّلَّذِينَ أَحۡسَنُواْ ٱلۡحُسۡنَىٰ وَزِيَادَةٞۖ وَلَا يَرۡهَقُ وُجُوهَهُمۡ قَتَرٞ وَلَا ذِلَّةٌۚ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَنَّةِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ ﴾
[يُونس: 26]
﴿للذين أحسنوا الحسنى وزيادة ولا يرهق وجوههم قتر ولا ذلة أولئك أصحاب﴾ [يُونس: 26]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ni ya Waumini, waliofanya vizuri kumuabudu Mwenyezi Mungu,wakamtii katika yale Aliyowaamrisha na Akayakataza, Pepo na zaidi yake ambayo ni kuutazama Uso wa Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, huko Peponi, na kupata msamaha na radhi. Na wala nyuso zao hazitafinikwa na vumbi wala unyonge kama itakavyo kuwapata watu wa Moto. Hawa wanaosifika na sifa hizi ndio watu wa Peponi, ni wenye kukaa milele kabisa humo |