Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 28 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَيَوۡمَ نَحۡشُرُهُمۡ جَمِيعٗا ثُمَّ نَقُولُ لِلَّذِينَ أَشۡرَكُواْ مَكَانَكُمۡ أَنتُمۡ وَشُرَكَآؤُكُمۡۚ فَزَيَّلۡنَا بَيۡنَهُمۡۖ وَقَالَ شُرَكَآؤُهُم مَّا كُنتُمۡ إِيَّانَا تَعۡبُدُونَ ﴾
[يُونس: 28]
﴿ويوم نحشرهم جميعا ثم نقول للذين أشركوا مكانكم أنتم وشركاؤكم فزيلنا بينهم﴾ [يُونس: 28]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kumbuka, ewe Mtume, Siku ambayo tutawafufua viumbe wote ili wahesabiwe na walipwe, kisha tuseme kuwaambia waliomshirikisha Mwenyezi Mungu, «Jilazimisheni mahali mliopo, nyinyi na washirika wenu ambao mlikuwa mkiwaabudu badala ya Mwenyezi Mungu, mpaka tuangalie mtafanya nini.» Hapo tutapambanua baina ya washirikina na wale wanaowaabudu, na watajitenga, wale walioabudiwa badala ya Mwenyezi Mungu, na wale waliokuwa wanawaabudu, na watasema kuwaambia washirikina «Hamkuwa mkituabudu sisi ulimwenguni.» |