Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 60 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَمَا ظَنُّ ٱلَّذِينَ يَفۡتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلۡكَذِبَ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَذُو فَضۡلٍ عَلَى ٱلنَّاسِ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَهُمۡ لَا يَشۡكُرُونَ ﴾
[يُونس: 60]
﴿وما ظن الذين يفترون على الله الكذب يوم القيامة إن الله لذو﴾ [يُونس: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hawa wanaomzulia Mwenyezi Mungu urongo, wakamnasibishia uharamishaji wa vitu ambavyo Yeye Hakuviharamisha kati ya riziki na vyakula, wanadhani kuwa Mwenyezi Mungu Atawafanya nini Siku ya Kiyama, siku ya wao kuhesabiwa, kwa urongo wao waliomzulia? Je,wanadhani kwamba Yeye Atawaacha na Atawasamehe? Mwenyezi Mungu Ana wema mwingi kwa viumbe Wake kwa kuacha Kwake kuyaharakisha mateso duniani kwa aliyemzulia urongo, na badala yake kumpa muhula. Lakini wengi zaidi wa watu hawamshukuru Mwenyezi Mungu kwa wema wake juu yao kwa hilo |