Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 64 - يُونس - Page - Juz 11
﴿لَهُمُ ٱلۡبُشۡرَىٰ فِي ٱلۡحَيَوٰةِ ٱلدُّنۡيَا وَفِي ٱلۡأٓخِرَةِۚ لَا تَبۡدِيلَ لِكَلِمَٰتِ ٱللَّهِۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلۡفَوۡزُ ٱلۡعَظِيمُ ﴾
[يُونس: 64]
﴿لهم البشرى في الحياة الدنيا وفي الآخرة لا تبديل لكلمات الله ذلك﴾ [يُونس: 64]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Mawalii hawa wana bishara njema kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa watapata ya kuwafurahisha katika maisha ya kilimwengu, na miongoni mwayo ni ndoto njema anayoiona mwenyewe au akaonewa na duguye, na watapata Pepo kesho Akhera. Mwenyezi Mungu Haendi kinyume na ahadi Yake wala Haigeuzi. Huko ndiko kufaulu kukubwa, kwa kuwa bishara hiyo imekusanya kuokoka na kila lifanyiwalo hadhari na kufaulu kupata kila litakwalo na kupendwa |