Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 65 - يُونس - Page - Juz 11
﴿وَلَا يَحۡزُنكَ قَوۡلُهُمۡۘ إِنَّ ٱلۡعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًاۚ هُوَ ٱلسَّمِيعُ ٱلۡعَلِيمُ ﴾
[يُونس: 65]
﴿ولا يحزنك قولهم إن العزة لله جميعا هو السميع العليم﴾ [يُونس: 65]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na yasikusikitishe, ewe Mtume, maneno ya washirikina juu ya Mola wao na kumzulia kwao Yeye urongo na kuishirikisha kwao mizimu ya masanamu pamoja na Yeye. Kwani Mwenyezi Mungu Ndiye Aliyepwekeka kwa nguvu zilizokamilika na uwezo uliotimia, ulimwenguni na Akhera; na Yeye Ndiye Msikizi wa maneno yao Ndiye Mjuzi wa nia zao na matendo yao |