Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 67 - يُونس - Page - Juz 11
﴿هُوَ ٱلَّذِي جَعَلَ لَكُمُ ٱلَّيۡلَ لِتَسۡكُنُواْ فِيهِ وَٱلنَّهَارَ مُبۡصِرًاۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَأٓيَٰتٖ لِّقَوۡمٖ يَسۡمَعُونَ ﴾
[يُونس: 67]
﴿هو الذي جعل لكم الليل لتسكنوا فيه والنهار مبصرا إن في ذلك﴾ [يُونس: 67]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Yeye Ndiye Ambaye Amewaekea nyinyi, enyi wtu, usiku ili mtuliye ndani yake na mpumzike na usumbufu wa harakati za kutafuta maisha , na Amewaekea mchana ili muone ndani yake na muende mbio kutafuta riziki yenu. Hakika katika kupishana usiku na mchana na hali ya watu katiaka vipindi viwili hivyo pana dalili na hoja, kwa watu wanaozisikia hoja hizi na kuzitafakari, kwamba Mwenyezi Mungu, Peke Yake, Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa |