×

Wamesema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu, Aliye takasika! Yeye ni Mkwasi, Mwenye 10:68 Swahili translation

Quran infoSwahiliSurah Yunus ⮕ (10:68) ayat 68 in Swahili

10:68 Surah Yunus ayat 68 in Swahili (السواحيلية)

Quran with Swahili translation - Surah Yunus ayat 68 - يُونس - Page - Juz 11

﴿قَالُواْ ٱتَّخَذَ ٱللَّهُ وَلَدٗاۗ سُبۡحَٰنَهُۥۖ هُوَ ٱلۡغَنِيُّۖ لَهُۥ مَا فِي ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِي ٱلۡأَرۡضِۚ إِنۡ عِندَكُم مِّن سُلۡطَٰنِۭ بِهَٰذَآۚ أَتَقُولُونَ عَلَى ٱللَّهِ مَا لَا تَعۡلَمُونَ ﴾
[يُونس: 68]

Wamesema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu, Aliye takasika! Yeye ni Mkwasi, Mwenye Kujitosheleza. Vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi ni vyake peke yake. Nyinyi hamna uthibitisho wowote wa haya! Mnamzulia Mwenyezi Mungu msiyo yajua

❮ Previous Next ❯

ترجمة: قالوا اتخذ الله ولدا سبحانه هو الغني له ما في السموات وما, باللغة السواحيلية

﴿قالوا اتخذ الله ولدا سبحانه هو الغني له ما في السموات وما﴾ [يُونس: 68]

Abdullah Muhammad Abu Bakr
Washirikina walisema, «Mwenyezi Mungu amejifanyia mwana» kama vile wanavyosema: ‘Malaika ni watoto wa kike wa Mwenyezi Mungu’, au ‘Al-Masīh( ni mwana wa Mwenyezi Mungu’. Mwenyezi Mungu Ametakasika na hayo yote na Ameepukana nayo! Yeye Ndiye Mkwasi Asiyemuhitajia kila asiyekuwa Yeye. Ni Vyake Yeye vyote vilivyoko kwenye mbingu na ardhi. Vipi basi Atakuwa na mwana miongoni mwa Aliyewaumba na hali ni kwamba kila kitu kinamilikiwa na Yeye? Na nyinyi hamuna dalili yoyote juu ya urongo mnaouzua. Je, mnasema kuhusu Mwenyezi Mungu maneno msiyoyajua ukweli wake na usawa wake)
❮ Previous Next ❯

Verse in more languages

Transliteration Bangla Bosnian German English Persian French Hindi Indonesian Kazakh Dutch Russian Spanish Turkish Urdu Uzbek