Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 1 - هُود - Page - Juz 11
﴿الٓرۚ كِتَٰبٌ أُحۡكِمَتۡ ءَايَٰتُهُۥ ثُمَّ فُصِّلَتۡ مِن لَّدُنۡ حَكِيمٍ خَبِيرٍ ﴾
[هُود: 1]
﴿الر كتاب أحكمت آياته ثم فصلت من لدن حكيم خبير﴾ [هُود: 1]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Alif, Lām, Rā’. Maneno yashatangulia, kuhusu herufi zinazokatwa, katika mwanzo wa Sura ya Al-Baqarah. Hiki ni Kitabu ambacho Mwenyezi Mungu Amemteremshia Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukiye, na ambacho aya zake zimepangwa vizuri zisizo na kasoro wala ubatilifu, kisha zimefafanuliwa kwa maamrisho na makatazo na maelezo ya halali na haramu yatokayo kwa Mwenyezi Mungu Aliye na hekima katika uendeshaji mambo Aliye Mtambuzi wa vile yanavyoishia |