Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 13 - هُود - Page - Juz 12
﴿أَمۡ يَقُولُونَ ٱفۡتَرَىٰهُۖ قُلۡ فَأۡتُواْ بِعَشۡرِ سُوَرٖ مِّثۡلِهِۦ مُفۡتَرَيَٰتٖ وَٱدۡعُواْ مَنِ ٱسۡتَطَعۡتُم مِّن دُونِ ٱللَّهِ إِن كُنتُمۡ صَٰدِقِينَ ﴾
[هُود: 13]
﴿أم يقولون افتراه قل فأتوا بعشر سور مثله مفتريات وادعوا من استطعتم﴾ [هُود: 13]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Au je, washirikina hawa, miongoni mwa watu wa Makkah, wanasema kwamba Muhammad ameizua hii Qur’ani? Waambie basi, «Iwapo mambo ni kama mnavyodai, leteni sura kumi mfano wake za kuzuliwa, na muwaite mnaowaweza miongoni mwa viumbe wote wa Mwenyezi Mungu, ili wawasaidie kuzileta hizi sura kumi, iwapo nyinyi ni wa kweli katika madai yenu |