Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 17 - هُود - Page - Juz 12
﴿أَفَمَن كَانَ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّهِۦ وَيَتۡلُوهُ شَاهِدٞ مِّنۡهُ وَمِن قَبۡلِهِۦ كِتَٰبُ مُوسَىٰٓ إِمَامٗا وَرَحۡمَةًۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُؤۡمِنُونَ بِهِۦۚ وَمَن يَكۡفُرۡ بِهِۦ مِنَ ٱلۡأَحۡزَابِ فَٱلنَّارُ مَوۡعِدُهُۥۚ فَلَا تَكُ فِي مِرۡيَةٖ مِّنۡهُۚ إِنَّهُ ٱلۡحَقُّ مِن رَّبِّكَ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يُؤۡمِنُونَ ﴾
[هُود: 17]
﴿أفمن كان على بينة من ربه ويتلوه شاهد منه ومن قبله كتاب﴾ [هُود: 17]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Je, yule aliyekuwa kwenye hoja na uangalifu kutoka kwa Mola wake katika kile anachokiamini na anachokilingania kwa wahyi ambao ndani yake Mwenyezi Mungu Ameuteremsha ushahidi huu, na ukafuatiwa na hoja nyingine kutoka Kwake yenye kuutolea ushahidi, nayo ni Jibrili au ni Muhammad, rehema na amani ziwashukie, na ukatiliwa nguvu na dalili ya tatu kabla ya Qur’ani, nayo ni Taurati - Kitabu alichotemshiwa Mūsā chenye uongozi na rehema kwa waliokiamini- (je yeye) ni kama yule ambaye hamu yake ilikuwa ni maisha yenye kutoweka na pambo lake? Hao wanaiamini hii Qur’ani wanazifuata hukumu zake kivitendo. Na mwenye kuikanusha hii Qur’ani, miongoni mwa wale waliojikusanya kumpinga Mtume wa Mwenyezi Mungu, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie, basi malipo yake ni Moto, hapana budi atauingia. Basi usiwe na shaka juu ya jambo la Qur’ani na kuwa inatoka kwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka baada ya dalili na hoja kulitolea ushahidi hilo. Na ujue kwamba Dini hii ndio ukweli unaotoka kwa Mola wako, lakini wengi wa watu hawaamini wala hawayatendi yale wanayoamrishwa. Huu ni muongozo unaowaenea ummah wa Muhammad, rehema ya Mwenyezi Mungu na amani zimshukie |