Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 18 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَمَنۡ أَظۡلَمُ مِمَّنِ ٱفۡتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًاۚ أُوْلَٰٓئِكَ يُعۡرَضُونَ عَلَىٰ رَبِّهِمۡ وَيَقُولُ ٱلۡأَشۡهَٰدُ هَٰٓؤُلَآءِ ٱلَّذِينَ كَذَبُواْ عَلَىٰ رَبِّهِمۡۚ أَلَا لَعۡنَةُ ٱللَّهِ عَلَى ٱلظَّٰلِمِينَ ﴾
[هُود: 18]
﴿ومن أظلم ممن افترى على الله كذبا أولئك يعرضون على ربهم ويقول﴾ [هُود: 18]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na hakuna yoyote aliye dhalimu zaidi kuliko yule aliyemzulia Mwenyezi Mungu urongo. Hao wataorodheshwa kwa Mola wao Siku ya Kiyama, ili Awahesabu kwa matendo yao. Na watasema waliohudhuria miongoni mwa Malaika na Manabii na wengineo, «Hawa ndio wale waliosema urongo kumsingizia Mola wao ulimwenguni. Mwenyezi Mungu Amewakasirikia wao na Amewalaani laana isiyokatika, kwa kuwa udhalimu walioufanya umekuwa ni sifa inayoambatana na wao |