Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 61 - هُود - Page - Juz 12
﴿۞ وَإِلَىٰ ثَمُودَ أَخَاهُمۡ صَٰلِحٗاۚ قَالَ يَٰقَوۡمِ ٱعۡبُدُواْ ٱللَّهَ مَا لَكُم مِّنۡ إِلَٰهٍ غَيۡرُهُۥۖ هُوَ أَنشَأَكُم مِّنَ ٱلۡأَرۡضِ وَٱسۡتَعۡمَرَكُمۡ فِيهَا فَٱسۡتَغۡفِرُوهُ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِۚ إِنَّ رَبِّي قَرِيبٞ مُّجِيبٞ ﴾
[هُود: 61]
﴿وإلى ثمود أخاهم صالحا قال ياقوم اعبدوا الله ما لكم من إله﴾ [هُود: 61]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Na tulimtuma kwenda kwa Thamūd ndugu yao Ṣāliḥ akasema kuwaambia, «Enyi watu wangu, muabuduni Mwenyezi Mungu, Peke Yake. Nyinyi hamuna mungu yoyote anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Yeye, Aliyetukuka na kuwa juu. Basi mtakasieni ibada. Yeye Ndiye Aliyeanza kuwaumba kutokamana na ardhi, kwa kumuumba baba yenu Ādam kutokamana na hiyo, na akawafanya nyinyi ni wenye kuiimarisha. Hivyo basi, muombeni Awasamehe madhambi yenu, na rudini Kwake kwa kutubia kidhati. Hakika Mola wangu yuko karibu na yule anayemtakasia ibada na akawa na hamu ya kuja Kwake kwa kutubia, ni Mwenye kumuitikia anapomuomba.» |