Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 60 - هُود - Page - Juz 12
﴿وَأُتۡبِعُواْ فِي هَٰذِهِ ٱلدُّنۡيَا لَعۡنَةٗ وَيَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِۗ أَلَآ إِنَّ عَادٗا كَفَرُواْ رَبَّهُمۡۗ أَلَا بُعۡدٗا لِّعَادٖ قَوۡمِ هُودٖ ﴾
[هُود: 60]
﴿وأتبعوا في هذه الدنيا لعنة ويوم القيامة ألا إن عادا كفروا ربهم﴾ [هُود: 60]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Wakafuatiwa, katika ulimwengu huu, na laana ya Mwenyezi Mungu, na wakafuatwa na hasira Zake Siku ya Kiyama. Jueni mtanabahi kwamba 'Ād walimkanusha Mola wao na wakawakanusha Mitume Wake. Jueni mtanabahi kwamba umbali na rehema ya Mwenyezi Mungu na maangamivu yatawashukia 'Ād, watu wa Hūd, kwa sababu ya ushirikina wao na kukanusha kwao neema ya Mola wao |