Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 63 - هُود - Page - Juz 12
﴿قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَءَاتَىٰنِي مِنۡهُ رَحۡمَةٗ فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ ٱللَّهِ إِنۡ عَصَيۡتُهُۥۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيۡرَ تَخۡسِيرٖ ﴾
[هُود: 63]
﴿قال ياقوم أرأيتم إن كنت على بينة من ربي وآتاني منه رحمة﴾ [هُود: 63]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Ṣāliḥ akasema kuwaambia watu wake, «Enyi watu wangu, iwapo niko kwenye hoja ya Mwenyezi Mungu na ukanijia mimi utume na hekima kutoka Kwake, niambieni mimi: ni nani atakayeniondolea adhabu ya Mwenyezi Mungu nikimuasi, nisiufikishe ujumbe na nisitoe ushauri mzuri kwenu? Hapo hamtaniogezea isipokuwa upotevu na kuwa mbali na wema |