Quran with Swahili translation - Surah Hud ayat 88 - هُود - Page - Juz 12
﴿قَالَ يَٰقَوۡمِ أَرَءَيۡتُمۡ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٖ مِّن رَّبِّي وَرَزَقَنِي مِنۡهُ رِزۡقًا حَسَنٗاۚ وَمَآ أُرِيدُ أَنۡ أُخَالِفَكُمۡ إِلَىٰ مَآ أَنۡهَىٰكُمۡ عَنۡهُۚ إِنۡ أُرِيدُ إِلَّا ٱلۡإِصۡلَٰحَ مَا ٱسۡتَطَعۡتُۚ وَمَا تَوۡفِيقِيٓ إِلَّا بِٱللَّهِۚ عَلَيۡهِ تَوَكَّلۡتُ وَإِلَيۡهِ أُنِيبُ ﴾
[هُود: 88]
﴿قال ياقوم أرأيتم إن كنت على بينة من ربي ورزقني منه رزقا﴾ [هُود: 88]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Akasema Shu'ayb, «Enyi watu wangu, Mwaonaje iwapo mimi niko kwenye njia iliyo wazi itokayo kwa Mola wangu katika yale ninayowaitia ya kumtakasia Yeye ibada, na katika yale ninayowakataza ya kuharibu mali, na Akawa Ameniruzuku riziki ya ukunjufu ya halali iliyo nzuri? Na sitaki kuenda kinyume na nyinyi, nikafanya jambo nililowakataza; na sitaki, katika niwaamrishalo na niwakatazalo, isipokuwa ni kuwarakibisha kadiri ya uweza wangu na kujimudu kwangu. Na kuafikiwa kwangu, katika kuipata haki na kujaribu kuwarakibisha, kuko kwa Mwenyezi Mungu. Kwake Yeye, Peke Yake, nimejitegemeza, na Kwake Yeye narejea kwa kutubia na kuelekea |