Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 111 - يُوسُف - Page - Juz 13
﴿لَقَدۡ كَانَ فِي قَصَصِهِمۡ عِبۡرَةٞ لِّأُوْلِي ٱلۡأَلۡبَٰبِۗ مَا كَانَ حَدِيثٗا يُفۡتَرَىٰ وَلَٰكِن تَصۡدِيقَ ٱلَّذِي بَيۡنَ يَدَيۡهِ وَتَفۡصِيلَ كُلِّ شَيۡءٖ وَهُدٗى وَرَحۡمَةٗ لِّقَوۡمٖ يُؤۡمِنُونَ ﴾
[يُوسُف: 111]
﴿لقد كان في قصصهم عبرة لأولي الألباب ما كان حديثا يفترى ولكن﴾ [يُوسُف: 111]
Abdullah Muhammad Abu Bakr Kwa hakika kwenye habari za Mitume tulizokuelezea na mambo yaliyowakumba wenye kukanusha kuna mawaidha kwa wenye akili timamu. Hii Qur’ani haikuwa ni habari ya urongo iliyozuliwa, lakini tumeiteremsha ikiwa ni yenye kutolea ushahidi ukweli wa vitabu vilivyoteremshwa vilivyotangulia na kwamba vinatoka kwa Mwenyezi Mungu, na ikiwa ni ufafanuzi wa kila ambalo waja wanalihitaji la kuhalalishiwa na kuharamishiwa, linalopendeza na linalochukiza na mengineyo, na ikiwa ni muelekezo kutoka kwenye upotevu na ni rehema, kwa wenye Imani, ya kuzifanya nyoyo zao ziongoke, wapate kuyafuata kivitendo maamrisho na makatazo yaliyomo |