Quran with Swahili translation - Surah Yusuf ayat 40 - يُوسُف - Page - Juz 12
﴿مَا تَعۡبُدُونَ مِن دُونِهِۦٓ إِلَّآ أَسۡمَآءٗ سَمَّيۡتُمُوهَآ أَنتُمۡ وَءَابَآؤُكُم مَّآ أَنزَلَ ٱللَّهُ بِهَا مِن سُلۡطَٰنٍۚ إِنِ ٱلۡحُكۡمُ إِلَّا لِلَّهِ أَمَرَ أَلَّا تَعۡبُدُوٓاْ إِلَّآ إِيَّاهُۚ ذَٰلِكَ ٱلدِّينُ ٱلۡقَيِّمُ وَلَٰكِنَّ أَكۡثَرَ ٱلنَّاسِ لَا يَعۡلَمُونَ ﴾
[يُوسُف: 40]
﴿ما تعبدون من دونه إلا أسماء سميتموها أنتم وآباؤكم ما أنـزل الله﴾ [يُوسُف: 40]
Abdullah Muhammad Abu Bakr «Nyinyi hamuabudu chochote kisichokuwa Mwenyezi Mungu isipokuwa ni majina yasiyokuwa na maana yoyote, mumeyafanya ni waola, nyinyi na baba zenu, kwa ujinga wenu na upotevu; Mwenyezi Mungu Hakuteremsha hoja au dalili yoyote juu ya usahihi wake. Hukumu ya haki ni ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, Peke Yake, Asiye na mshirika. Yeye Ameamrisha kwamba msimwandame wala msimnyenyekee Asiyekuwa Yeye, na kwamba mumuabudu Yeye Peke Yake. Na hii ndiyo Dini iliyolingana sawa isiyokwenda kombo. Lakini wengi zaidi wa watu hawalielewi hilo, hawaujui uhakika wake |